Copy
Jitihada za uhifadhi zaanza kuzaa matunda Tanzania, wanyamapori wakiongezeka
Na Peter Elias

Hifadhi ya Taifa ya Katavi ni hifadhi ya tatu kwa ukubwa nchini Tanzania na ni makazi ya maelfu ya wanyama. Ina ukubwa wa kilomita za mraba 4,471 na moja ya sifa kuu za hifadhi hii ni kuwa na viboko zaidi ya 5,400 na baadhi ya wanyama wakuu wa tano  yaaani simba Tembo, kifaru, Chui na Mbogo.

Tofauti na mbuga nyingine nyingi, mbuga hii ina historia ya kipekee kutokana na  asili yake na pia ina mkusanyiko wa  mito na maziwa mengi ambayo hutoa maji kusaidia wanyamapori.

Hifadhi hii ina wanyama pori zaidi ya 100,000 wanyama hao ni pamoja na  simba, chui, tembo, viboko, mamba, swala, nyati, twiga na pundamilia. Pia, Katavi ni makazi ya zaidi ya spishi 450 za ndege, wakubwa kwa wadogo

Kiboko wakiota jua kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Hazina hizi zinaifanya kuwa kivutio cha utalii na watu wa ndani na wageni wamekuwa wakitembelea hifadhi hiyo ili kuona wanyama wa aina mbalimbali, hasa viboko wanaoifanya hifadhi hii kuwa ya kipekee.

Francis Konde, Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi, anasema wanapokea watalii 3,800 kwa mwaka. “Watu wengi wanaotembelea hifadhi hiyo ni Watanzania wakifuatiwa na watu kutoka Marekani, Ujerumani, Ufaransa na Ubelgiji,” anasema.

Katavi, sawa na maeneo mengine ya hifadhi, ujangili wa wanyamapori ni changamoto kubwa. Hii ni kwa sababu mbuga hiyo haina uzio; kwa hiyo, mtu yeyote anaweza kuingia na kuua wanyama kwa urahisi ikiwa atabahatika kutoka bila kukamatwa.

Konde anafichua kuwa kuwepo kwa soko la meno ya tembo na nyara nyingine katika nchi za Asia kama China na Thailand kunachangia kwa kiasi kikubwa ujangili.

Hata hivyo, hifadhi hiyo imeboresha ufuatiliaji pamoja na ushiriki wa wananchi katika shughuli za uhifadhi, jambo ambalo limesaidia kupunguza usafirishaji wa wanyamapori katika miaka ya hivi karibuni.

Francis Konde, Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi,
Soma kikamilifu kwenye mtandao wa InfoNile
Mkurugenzi wa AWF Didi Wamukoya,   anasema juhudi za kupambana na ujangili wa tembo zimezaa matunda kwa sababu mauaji haramu ya tembo kwa ajili ya pembe za ndovu barani Afrika yamekuwa yakipungua tangu mwaka 2011.

Wamukoya anabainisha kuwa idadi ya tembo nchini Tanzania imekuwa ikiongezeka kwa kasi kutoka 43,000 mwaka 2014 hadi 60,000 mwaka 2019, kulingana na Ripoti ya Sensa ya Wanyamapori Tanzania ya 2019.
Tembo wa Kiafrika porini, Tanzania
Kupungua huku kwa uhalifu wa wanyamapori nchini Tanzania kumefuatiliwa kwenye #WildEye Afrika Mashariki, ramani mpya shirikishi iliyotolewa na InfoNile na Oxpeckers Investigative Environmental Journalism.

Kutoka kwa kesi 105 zilizofuatiliwa za uhalifu wa wanyamapori ambazo zilifunguliwa kati ya 2017-2022 nchini Tanzania, idadi kubwa ya wanyamapori walikamatwa wakati wa 2015-2016.
#InfoData
Wamukoya anasema kweli kumekuwa na kupungua kwa nyara nchini Tanzania. Anaongeza kuwa ukamataji unaweza kuwa wa endelevu kutokana na kuimarishwa kwa utekelezaji na kuundwa kwa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kupambana na Ujangili (NTAP) mwaka 2016, ambacho ni jukwaa la mashirika ya kusaidia kukabiliana na uhalifu wa wanyamapori.
Soma kwa Kiingereza

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ilianzishwa mwaka 2014 kwa lengo la kufanya doria za kupambana na ujangili ndani na nje ya Mapori ya Akiba na Maeneo ya hifadhi.

Kwa mujibu wa taarifa kwenye tovuti yao, tangu kuanzishwa kwa TAWA hadi Septemba 2016, jumla ya doria 69,278 zilifanyika ndani na nje ya Mapori ya Akiba na Maeneo Tawala na kusababisha kukamatwa kwa majangili 1,563.

Nyara zilizokamatwa ni pamoja na vipande 90 vya pembe za ndovu zenye uzito wa kilogramu 376.33  kilo 29, 529.5 za nyama ya wanyampori wa aina mbalimbali, bunduki 141 na risasi 278.

TAWA ina kitengo cha mbwa kinachosaidia katika ukaguzi wa mazao ya wanyapori kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na bandari ya Dar es salaam.

Soma kikamilifu kwenye mtandao wa InfoNile
Jibu kali la kisheria

Bi Wamukoya anabainisha kwamba kupungua kwa ujangili na usafirishaji wa tembo nchini Tanzania kumechangiwa na juhudi zinazofanywa za kutekeleza sheria zilizopo kwa kudhibiti makundi yanayo jihusisha na ujangili.

Pia anatoa shukurani zake kwa ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa katika kupiga vita ujangili na usafirishaji bidhaa za wanyama pori kwa kuwa  biashara hii ni ya kimataifa.

Kwa mujibu wa data zilizokusanywa na WidlifeEye East Africa nchini Tanzania, idadi kubwa ya watu waliopatikana na hatia ya uhalifu wa wanyapori walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.  

Pia Baadhi ya hukumu ziliambatana na faini au dhabu zinazolingana na thamani ya wanyapori waliokamatwa; hata hivyo adhabu zilikuwa chache ikilinganishwa waliowekwa kifungoni na hakukuwa na thamani ya kifedha ya adhabu iliyolingana kwa mtu aliyepatikana na hatia”
Mkurugenzi wa wanyamapori  kutoka Wizara ya Mali asili na Utalii bwana Maurus Msuha anasema ongezeko la tembo limechangiwa na mifumo mizuri ya ulinzi kwenye maeneo ya hifadhi. 
Maurus Msuha, Mkurugenzi wa wanyamapori, Wizara ya Mali asili na Utalii.

“Operesheni zetu tumeziweka kijeshi. Pia tuna mfumo mwingine unaozihusisha taasisi zingine; kwahiyo tuko vizuri kwenye ulinzi wa wanyamapori” anasema bwana Msuha. Pembe nyingi za Tembo zilizokamatwa hivi karibuni zina umri wa miaka sita au saba, hali inayoonyesha kuwa ujangili umepungua sana ikilinganishwa na miaka ya kabla ya mwaka 2014 ambapo maelfu ya Tembo waliuwawa kila mwaka.

Msuha anabainisha kuwa haya yote yanafanyika ili kuwalinda faru pia ambao idadi yao inaongeka kabla ya lengo lililowekwa.

 

“Kwa mujibu wa data zilizokusanywa hadi sasa na WildEye East Africa nchini Tanzania, takriban nusu ya kesi zote zinahusisha pembe za ndovu na asilimia 90 ya kesi hizi zilihusisha umiliki haramu wa pembe, nyama tembo na sehemu zingine za wanyama hawa.

#InfoData
Takwimu za Ujangili wa wanyamapori Tanzania, (2017- 2022)
Zaidi ya asilimia 90 ya bidhaa za wanyamapori zilizokamatwa nchini Tanzania kuanzia 2017 hadi 2022 zilikuwa ni za tembo.
Read more stories on InfoNile

Ujangili, tatizo linaloendelea

Pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali na wadau wengine kukomesha ujangili wa wanyapori, bado tatizo hili linaendelea. Kuna baadhi ya wahalifu wanawatumia wenyeji, walinzi wa wanyapori na hata wafanyabiashara kupata pembe za ndovu kutoka kwenye hifadhi za wanyama pori.

Bwana Msuha anasema bado kuna soko haramu kwenye nchi za asia kama vile Vietnam, Malaysia na nchi nyingine Mashariki mwa bara la Asia mbako watu wanaamini kuwa na mapambo yaliyo tengenezwa  kutokana na pembe za ndovu ni ishara ya utajiri.

Tembo malishoni

Hakimu wa mahakama ya Kisutu iliyoko jijini Dar es Salaam amekuwa akisikiliza kesi kadhaa zinazohusu ujangili na pembe za ndovu ambapo baadhi ya watu wamehukumiwa kwenda jela na wengine kuachiwa huru.

Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam wanawashikilia watu watatu wanaotuhumiwa kukutwa na vipande ishirini na tano vya meno ya tembo kwenye opresheni maalum iliyofanyika maeneo ya Magomeni na Manzase Jijini Dar es Salaam.

Mapema mwaka huu Hakimu mkazi wa mahakama ya Kisutu alimhukumu bi Haika Mgao mwenye umri wa 26 kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukutwa na hatia kukutwa na vipande vya pembe za ndovu na meno ya kiboko yenye thamani shilimgi za kitanzania millioni 69.5 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Soma kikamilifu kwenye matandao wa InfoNile
Usaidizi wa  ukuzaji na utengenezaji wa hadithi hii ulitoka kwa InfoNile, kwa ushirikiano na Oxpeckers Investigative Environmental Journalism, kwa ufadhili wa Earth Journalism Network. Vielelezo vya data na Ruth Mwizeere na Annika McGinnis / InfoNile.
Share Share
Tweet Tweet
Forward to a friend Forward to a friend
Facebook
Twitter
Link
Website






This email was sent to <<Email Address>>
why did I get this?    unsubscribe from this list    update subscription preferences
InfoNile.org · 5th Street Industrial Area PO Box 7381, Kampala UGANDA · Kampala · Uganda